Maumivu Ya Tumbo Katikati Ya Mzunguko Wa Hedhi


Je unapata maumivu ya tumbo chini ya kitovu au kwenye kinena siku za katikati ya mzunguko?.kama unapata hali hii unapata hali kitaalam inaitwa MITTELSCHMERZ.

MITTELSCHMERZ ni maumivu yanayotokea kwenye   tumbo sehemu ya chini ya kitovu,kwenye kinena au kwenye nyonga kipindi unapokuwa siku za katikati ya mzunguko.yaani siku ambazo yai linakaribia kuachiliwa au linapoachiliwa kutoka kwenye vifuko vya mayai (ovari)

Kwa lugha nyingine tunaweza kusema ni maumivu ya tumbo na nyonga wakati wa siku za hatari.
Asilimia 20% ya wanawake wanapatwa na hali hii.

CHANZO
Kikawaida kwa mwanamke yai huachiliwa wiki 2 tokea kuanza kwa hedhi.mabadiliko ya hormone yanayotokea kipindi hiki huchochea mifuko ya mayai (ovari) na kupelekea kufanya yai lililokomaa kupasua utando unaolizunguka ili liachiliwe kutoka kwenye mfuko wa yai (ovari). Yai hili linatoka na majimaji yaliyokuwa yanalizunguka na pia damu.

Kitendo cha yai kupasua utando ili litoke hupelekea maumivu kidogo ya tumbo (mittelschmerz)

Pia maji maji yanayotoka pamoja na yai kutoka kwenye ovari yanaweza kusababisha kuta za mirija ya uzazi (fallopian tubes) kupata michomo (inflammations) na kupelekea kupata maumivu haya.

DALILI
Mamivu mithili ya kichomi au tumbo kukaza sehemu ya chini ya kitovu. halii pia inaweza kuambatana na kuona damu kidogo ukeni (spotting),hali hii uisha ndani ya masaa 24 hadi 48.

MATIBABU
Hali hii sio tatizo la kiafya, ni hali inayotokana utendaji kazi wa mfumo wa uzazi.

Unaweza kutumia njia zifatazo kupunguza hali hii inapokupata;
1.Kujikanda tumbo sehemu ya chini ya kitovu na maji ya moto inasaidia kuondoa/kupunguza hali hii

2.Kutumia dawa za kutuliza maumivu
3.Massage ya tumbo

Muda gani umwone daktari
1.Endapo maumivu ni makali sana
2.Imeambatana na homa
3.Hali hii ikitokea kwa muda unaozidi siku 3
4.Ikiambatana na kutoka uchafu ukeni wenye harufu.


EmoticonEmoticon