Messi Atwaa Tuzo Fifa

Leo Messi
Lionel Messi ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa  duniani inayotolewa na Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), katika hafla iliyofanyika September 23 usiku mjini Milan, Italia.

Hata hivyo, mpinzani wake Cristiano Ronaldo wa Juventus, hakuhudhuria utoaji wa tuzo hiyo.

Lionel Messi
Beki wa Liverpool, Virgil van Dijk aliyekuwa akipewa nafasi ya kutwaa tuzo hiyo alishika nafasi ya pili na Ronaldo ya tatu.

Messi alimpigia kura mshambuliaji  wa Liverpool na Senegal, Sadio Mane  akimtaja ndiye mchezaji wake bora duniani kuliko Ronaldo na Van Dijk.
Messi, Mke na Watoto Wake
Ronaldo alimpigia kura beki wa Juventus, Matthijs de Ligt na Van Dijk alimchagua Messi na nafasi ya pili alimpa Mohamed Salah.

Hii ni mara ya sita nahodha huyo wa Barcelona kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, ambapo amewahi kutwaa 2009, 2010, 2011, 2012 na 2015.


EmoticonEmoticon