Kuna Uwezekano Wa Samatta Kuikosa Mechi Ya Leo

Mshambuliaji na nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta kupitia klabu yake ya Genk ya Ubelgiji amefanikiwa kufuzu kutinga hatua ya makundi, lakini hii leo anaweza kuukosa mchezo wa kwanza kutokana na majeraha aliyoyapata hivi karibuni.

Jumapili ya Septemba 8, Samatta alikuwa akiiongoza Tanzania kwenye mchezo dhidi ya Burundi wa kufuzu makundi ya kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia.

Japo Tanzania ilishinda mchezo huo kwa mikwaju ya penati, Samatta alipata majeraha ya goti.

Taarifa rasmi ya majina ya wachezaji watakaocheza katika mchuano huo wa leo usiku bado haijatolewa, na itakapotolewa ndipo Watanzania watahakikisha kama Samatta atashuka dimbani leo ama watasubiri mchezo ujao kumuona ndani ya Champions League.


EmoticonEmoticon