Mwanamke Aliyetoa Dhamana Ya R Kelly Ataka Arudishiwe Pesa Zake

Mwanamke mmoja ambaye alijitoa kutoa fedha kwa ajili ya dhamana ya msanii R Kelly ataka arudishiwe pesa zake.

Mwanamke huyo ambaye alitoa kiasi cha zaidi ya milioni 70 kwa pesa za kitanzania ameiambia Mahakama siku ya jana kuwa anahitaji arudishiwe pesa zake kwani alifanya kwa makubaliano na baadhi ya wanafamilia wa R Kelly lakini wameshindwa kumrudishia kwa wakati.

Mwanadada huyo alitoa pesa hiyo kama dhamana kwa msanii R Kelly kutokana na kesi zake za unyanyasani wa kingono kwa wasichana wenye umri mdogo, kesi ambazo bado anaendelea kukabiliana nazo.


EmoticonEmoticon