Neymar Athibitisha Yeye Na PSG ni Damu Damu, Haendi Mahali

Neymar Jr
Neymar aliyekuwa akiwaniwa na Barcelona na Real Madrid mwanzoni mwa msimu huu, ameibuka na kauli ya kuwafurahisha mashabiki akisema hana mpango wa kuondoka PSG.

"Nina furaha ninapokuwa uwanjani na kuisaidia PSG kufanya vizuri, ni jambo zuri pamoja na mashabiki wetu," alisema.

"Hii ni kama vile unapokuwa na mchumba wako, kuna wakati unakua mbaya kwenu, lakini kumbatio na mapenzi ya dhati inakuwa vizuri," alisema Neymar.

Neymar aliongeza anataka maisha yake yawe PSG, na anataka kuhakikisha anaisaidia timu hiyo kutwaa mataji zaidi.


EmoticonEmoticon