Post Malone Album Yake Kuongoza Billboard

Album mpya ya Post Malone 'Hollywood's Bleeding' kukamata namba 1 kwenye chart za album Billboard 200 wiki ijayo. 
Album hiyo ya 3 kwa Malone imekadiriwa kuwa itafikisha jumla ya mauzo 500,000 katika wiki yake ya kwanza.

Mauzo haya yatamfanya Post Malone kukamata nafasi ya Pili kwenye orodha ya mauzo makubwa ya album kwa wiki mwaka 2019, namba 1 inakamatwa na 'Lover' ya Taylor Swift. Hollywood's Bleeding ilitoka September 6, 2019 na kuwapa shavu wakali kama Travis Scott, SZA, na Future.


EmoticonEmoticon