Rapa T.I Amaliza Beef Kati Yake Na Kanye West

Kanye West & T.I
Ibada ya Kanye West Jumapili hii mjini Atlanta imemuingia vizuri T.I. kwani ameamua kuimaliza bifu yake na rapper huyo.

Kupitia instagram akaunti yake, T.I ameandika kwamba licha ya yote ambayo yanaendelea kati yao, atabaki kuwa Kaka yake. Anafurahi kumuona akiwa amerejea kwenye Kanye yule wa zamani. Jumapili hii TIP alikuwa mgeni wa ibada hiyo ambayo huwakutanisha baadhi ya watu maarufu na wa kawaida kuimba na kusali pamoja.
T.I Instagram Post
Tukukumbushe tu, baada ya Kanye kutangaza rasmi upande wake kisiasa kwamba anamuunga mkono Rais Donald Trump, halikuwa tamko zuri kwa watu weusi na kilikuwa kidonge kichungu lakini T.I. aliamua kumvua nguo kwa kuandika:

"Hii ni kati ya vitendo vya aibu na fedheha kuwahi kushuhudia kwa mtu kuuza roho yake ili kujipatia nafasi fulani kwenye dola. Katika nyakati fulani, ilikuwa fahari kufanya kazi na pamoja na wewe, lakini sasa ninasikia aibu hata kuwahi kushirikiana na wewe." aliandika T.I. mwezi October 2018.


EmoticonEmoticon