Sababu 5 Zinazochangia Condom Kupasuka Wakati Wa Kufanya MapenziCondom za kiume ni condom pekee ambazo zimekua zikitumika kwa wingi kutokana na upatikanaji wake kua rahisi ,bei yake ni ndogo kulinganisha na condom nyinginezo.

Hivyo zimekua zikisaidia kuzuia mimba zisizo tarajiwa,kuzuia magonjwa ya zinaa na vilevile kuzuai maambukizi ya VVU.

Zifuatazo ni sababu 5 ambazo zinaweza kupelekea condom hizo kupasuka wakati wa tendo la ndoa..

1.Kama condom tayari imesha expire.

2.Kama zikihifadhiwa mahala penye mgandamizo mkubwa au mahala penye joto jingi mfano kwenye wallet nk unashauriwa kuhifadhi condom kwenye droo za kabati au droo za kitanda au mahala penye halijoto ya wastani.

3.Kama condom imepungukiwa vilainishi:Mara nyingi condom huja na mafuta yake ambayo hua kama kilainishi inapotokea vilainishi hivyo vimepungua huongeza msuguano na kupelekea condom kupasuka.

4.Condom kua kubwa kuliko uume au ndogo kuliko uume hii husababisha mpira huo kujiviringisha na kupelekea mpasuko.

5.Maumbile ya mwanamke:Kuna baadhi ya wanawake wana maumbile ya uke madogo hali hii husababisha misuli ya uke kuubana uume na kusababisha kupasuka kwa condom hyo hivyo unashauriwa kuongeza vilainishi ili kuzuia hadha hiyo.


EmoticonEmoticon