Sababu Na Tiba Ya Michirizi Ya Mwili Kwenye Ngozi


Katika ngozi ya baadhi ya watu, kuna aina Fulani ya mistari ambayo huonekana kama alama iliyobaki baada ya mtu kuumia, huonekana kama kovu, lakini siyo kovu na wala mtu hakupata ajari au kuumizwa na kitu chochote.

Mara nyingi alama hizi za michirizi humtokea mtu maeneo ambayo kwa asilimia kubwa huwa na mafuta (fat), mfano katika mwili hutokea mara nyingi kwenye mapaja, upande wa juu wa mikono (biceps), tumboni, kwenye makalio, pia kwa baadhi ya watu hutokea maeneo ya kifuani au kwenye matiti kwa wanawake.


VISABABISHI
Michirizi hii hutokana na kutanuka kwa ngozi na ongezeko la hormone ya Cortisone  ambayo inazalishwa na tezi zilizopo kwenye figo kitaalamu zinajulikana kama adrenal glands.Hormone hii huathiri uwezo wa ngozi kutanuka na kusinyaa.

Vitu gani vinaweza kupelekea tatizo hili.
1.Wakati wa ujauzito kutikana na ngozi ngozi ya tumbo kutanuka kwa kasi kuendana na ukubwa wa tumbo na mtoto.
2.Michirizi hii inaweza kutokea pale unapoongezeka uzito au kupungua kwa kasi
3.Matumizi ya dawa za kupaka (cream) zilizo katika group la CORTICOSTEROID Mfano Carolight kwani hizi huathiri uwezo wa ngozi kutanuka na kusinyaa.
4.Magonjwa mfano Cushing's syndrome,marfans syndrome na ehlers danlos syndrome.

WATU GANI WAKO KWENYE HATARI YA KUPATA TATIZO HILI
1.Wanawake wanene
2.Wajawazito
3.Watu wenye ngozi nyeupe
4.Wajawazito
5.Kubeba mimba ya mapacha
6.Kupungua uzito kwa kasi
7.Wanaotumia cream zenye Corticosteroids.

MATIBABU
Michirizi hii hupotea baada ya muda fulani, ila inachukua muda mrefu sana.zipo dawa mbali mbali ambazo zinaweza kutibu tatizo hili ila inahitajika kutumika kwa muda mrefu ili kupata matokeo.

Dawa hizi ni kama ifatavyo;
1.Tretnoin cream
Hii hufanya kazi kwa kuipatia ngozi protini aina ya collagen ambayo ndo inahusika katika kuweka sawa uwezo wa ngozi kusinyaa na kutanuka.
2.Pulse dye laser therapy hii ni tiba ya kutumia mionzi
3.Microdermabrasion

Pia matumizi ya mafuta ya kujipakaa yenye mchanganyiko wa vitamini E husaidia kuijenga ngozi na kutoa makovu na michirizi. Ulaji wa vyakula na kunywa vinywaji vyenye vitamini A, D na E huimarisha ngozi.

MATIBABU YA NYUMBANI
1.Kupaka mafuta ya nazi kwenye sehemu iliyoathirika husaidi kwenye tatizo hili
2.Aloevera,kwa kupaka maji maji ya mmea wa aloevera husaidia kutibu tatizo hili.Mafuta ya Aloe vera, pakaa mafuta haya katika ngozi yenye michirizi, pia unaweza kuyachanganya na vitamini A na ukapakaa ngozi yako.

3.Sukari
Sukari inatumika kwa kufanya scrub katika shemu iliyoathiriwa na tatizo hili. Fanya kama ifatavyo.
1.Changanya sukari na mafuta ya nazi au almond oil
2.Ongezea maji ya limao
3.Scrub eneo lililoathirika kwa muda wa dakika 8 hadi 10.
4.Fanya hivi angalu mara tatu kwa wiki.

4.VIAZI MVIRINGO
Tumia vipande vidogo vidogo vya viazi kufuta sehemu ya ngozi yenye michirizi, ruhusu juisi au maji maji ya kwenye viazi yakae katika ngozi, na kisha baadae unaweza kuosha ngozi yako kwa maji ya vuguvugu, kwani viazi vina madini na vitamini ambazo zikinyonywa katika ngozi, husaidia kuondoa michirizi


EmoticonEmoticon