Sababu Za Ugonjwa Wa Kujihisi Kizunguzungu

Moja ya malalamiko ya kiafya yanayowapata watu na kwenda hospitalini ni kizunguzungu. 

Kizunguzungu ni hali ya kuhisi kama vile vitu vilivyoko karibu nawe vinazunguuka (vertigo) au kusikia kichwa chepesi au kukosa uwiano (balance) na kujikuta mtu anapepesuka. 

Kwa aliyelala atahisi kitanda kinayumba yumba au kuzunguuka.

Kwa kuwa na kizunguzungu kunaweza kukaathiri shughuli zako za kila siku. Lakini pia ni mara chache sana kizunguzungu kikawa ni dalili za tatizo linalo hatarisha maisha.

Watu wanaopata kizunguzungu wana namna mbalimbali za kuelezea dalili zake, mfano:

· Kuhisi kama kichwa au mwili mzima unazunguuka
· Hali ya kujisikia kama unataka kupoteza fahamu au kichwa kuwa chepesi
· Kukosa balance
· Kuhisi kama unaelea angani au kwenye maji

Sababu  zinazoleta kizunguzungu

· Magonjwa ya mishipa ya fahamu
· Dawa zinazotumika kutibia matatizo mbalimbali yanaweza kuwa chanzo cha kizunguzungu. Mfano dawa za kuzuia degedege, dawa za sonona, na dawa za kutibu shinikizo la damu pia huwa ni sababu kwani kuna wakati hushusha shinikizo la damu kufikia chini ya kiwango.

· Aina fulani ya magonjwa yanayomfanya mtu kuwa na wasiwasi kuliko kawaida huleta kizungunguzu.

· Upungufu wa damu. Kupungua kwa wekundu wa chembechembe nyekundu za damu huleta kizungunguzu kwani kiwango cha hewa ya oxygen kinachozunguuka kinakuwa kidogo.

· Kushuka kwa sukari. Hali hii huwapata watu wenye kisukari wanaotumia insulin ambayo inaweza kusababisha sukari kushuka sana. Pia hata wenye njaa kupita kiasi.

· Joto kali na kupungukiwa maji. Joto kali husababisha kutokwa na jasho jingi hivyo maji mwilini kupungua na kuleta kizunguzungu.


EmoticonEmoticon