Taarifa Mpya Kuhusiana Na Kutoka Kwa Album Ya Gospel Ya Kanye West

Kanye West
Baada ya kusubiriwa album ya Jesus Is King toka kwa Kanye West ambayo ilikuwa itoke ijumaa ila ikasogezwa jumapili kwa mujibu wa Kim Kardashian, right now kuna taarifa kamili zimekuja kutokana na album hiyo kuchelewa sokoni

Kwa mujibu wa TMZ wameripoti kutoka kwa chanzo cha karibu cha Kanye ni kwamba album  hiyo imekwishakamilika ila Kanye hataki kuiachia kutokana na kila wakati anapoisikiliza anahitaji kubadilisha baadhi ya vitu kwenye album hiyo. Hakuna tarehe wala muda maalumu wa album hiyo kutoka ila itatoka muda na saa yoyote so watu wawe na subira.

Ye alifanya Listening Party ya album yake hiyo mjini Chicago jana Jumapili na alisikika akitangaza kuachana na muziki wa kidunia mbele ya wahudhuriaji. 


EmoticonEmoticon