Taarifa Mpya Za De Gea Kusaini Mkataba Mpya

De Gea Akisaini Mkataba

Kipa wa Manchester United David de Gea ametia saini mkataba mpya kusalia klabuni humo hadi mwaka 2023.

De Gea amechezea United mechi 367 tangu Sir Alex Ferguson kumleta klabuni humo kutoka Atletico Madrid kwa mkataba wa pauni milioni 18.9 Juni mwaka 2011.
De Gea Asaini Mkataba Mpya
De Gea, ambaye amechezea nchi ya Uhispania kwa mara 40, amesaidia United kushinda taji la ligi ya Pemier mwaka 2012-13, kombe la FA misimu mitatu baadae na pia kombe la ligi na ligi ya Uropa mwaka 2016-17.

Muhispania huyo ambaye amehusishwa na kuhamia Real Madrid hivi majuzi ,alikua katika mwaka wake wa mwisho wa mkataba.


EmoticonEmoticon