Wanasema kuwa ikiwa katika kipindi cha mwezi moja mtu yeyote
alitumia mchanganyiko wa tangawizi, limao ,asali, maji baridi na vitunguu saumu
na maji ya moto huenda amepata sumu hiyo.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa vipimo vya maabara kutoka maabara ya
serikali ya Kenya tani 23,000 za tangawizi zilizonunuliwa kutoka Vietnam
zilikuwa zimeoza, chafu na zenye unyvunyevu, na ukungu, limeripoti gazeti la
Sunday Nation nchini humo.
Bwana
Muhammed Duba Katibu mkuu wa Muungano wa Maafisa wa Afya, amesema kutokana na
matokeo ya maabara mzigo huo ulikuwa na ukungu" na tukaamua kuwa hawapaswi
kuupeleka sokoni ".
"Tumegundua kuwa tangawizi hizo ziliachiliwa ,huku zikiwa na
sumu ya aflatoxins. Tulielezea hofu zetu kwa maafisa kwamba tangawizi hizo
hazifai kuuzwa ," Alisema Bwana Duba.
Kutokana na hayo maafisa wa afya wanatoa onyo dhidi ya matumizi ya
sumu ambayo ilibainika kuwa kuharibu seli za ini na kusababisha saratani.
Mzigo
huo uliingizwa nchini na wafanyabiashara chini ya kampuni ya Fairoils EPZ
Limited mjini Nairobi katika kontena nambari number EGSU50117342 kwa madhumuni
ya kutengeneza mafuta.
Lakini uliachiliwa na kuingia hadi masokoni.
Agizo hilo linawataka maafisa wa afya ya umma kutoa ombi la kupata
idhini kutoka kwa Halmashauri ya kukagua ubora wa bidhaa nchini Kenya kabla ya
kufanya uchunguzi.
"tunahudumu katika bandari hii kwa mujibu wa sheria, sawa na
wao, na majukumu yetu ni tofauti. Kwanini tuandike barua ya kutaka tupewe
idhini ya kufanya uchunguzi?" Bw. Duba aliuliza.
Wamesema
kuwa maafisa wa afya ya umma ni wamepewa dhamana ya kulinda kifungu cha 242 cha
sheria ya afya ya umma kinachowapatia jukumu la kuwahakikishia wakenya usalama
wa chakula.
Kabla ya kutolewa kwa kutolewa kwa angalizo hilo la mwezi Juni,
jukumu kuu la afisa wa afya ya umma lilikuwa ukaguzi wa chakula na kutoa agizo
la kuharibiwa vile ambavyo havijafikia viwango vilivyowekwa.
Chama hicho kimeenda mahakamani kuomba agizo hilo lichunguzwe upya
ili warudishiwe jukumu lao la awali.
"tumewasilisha
ombi letu na kuhoji kuwa taifa liko katika hatari ya kukumbwa na kemikali
zisizo salama na chakula," Bw.Duba alisema, huku akiongeza kuondolewa kwa
jukumu hilo kutoka kwao limetokana na sababu za kibinafsi kutoka kwa wadau
wanaotaka kujifaidi bila kujali usalama wa Wakenya.
Shehena ya tangawizi inayokumbwa na utata iliwasili katika bandari
ya Mombasa na ilichunguzwa na maafisa wa afya ya umma mnamo Agost 8.
EmoticonEmoticon