Unahitaji Usingizi Wa Muda Gani?Muda Na Usingizi Unaohitajika Soma Hapa

Kuna tofauti kati kubwa kati ya kiwango cha usingizi unachopata na kuweza kufanya kazi zako na kiwango halisi ulichostahili kukipata ili kufanya kazi zako kiufanisi. Watu wengi sasa hivi hupata chini ya saa 7 za usinigizi na kwenye dunia ya leo yenye changamoto nyingi za kimaisha saa 6 au 7 huonekana kama ni kiwango sahihi cha usingizi. 

Ukweli ni kuwa hii ni kujiweka kwenye hali ya kuishia kwenye tatizo sugu la kukosa usingizi wa kutosha.

Kwa sababu tu unaweza kwenda kwa saa 6 au 7 za usingizi haimaanishi kuwa hungefanya kazi zako vizuri zaidi iwapo ungepata saa moja au mbili zaidi kitandani. Tebo ya hapa chini inaonyesha viwango elekezi vya muda wa usingizi kwa makundi mbalimbali.Njia bora ya kujua kama unapata usingizi kwa kiwango cha kutosha ni kujitathmini jinsi unavyojisikia pale unapoanza shughuli zako asubuhi. Kama unapata usingizi wa kutosha, utajisikia kuwa na nguvu na mchangamfu siku nzima kuanzia ulipoamka hadi utakapokwenda kulala.


EmoticonEmoticon