VIRUTUBISHO MUHIMU VYA KUBORESHA NGUVU ZA KIUME

Katika  kuangalia uwezo wa mbegu kulifikia yai tunaangalia mbegu kiasi gani zinatembea. Inapaswa angalau asilimia 60 ya mbegu zilizolishwa ziwe znatembea ndo unaweza kutungisha mimba

Kitu cha tatu ni kuangalia mbegu kama zina umbo sawa (morphology). Kwa kawaida mbegu ambazo zinakua haziko sawa zinakua na matatzo kwenye sehemu ya kichwa. 

Na kikawaida kati ya mbegu zote angalau asilimia 30% kuendelea ya mbegu inapaswa iwe na umbo la kawaida ( normal morphology),Ili kuweza kutungisha mimba. Kipimo wanachotumia wataalamu kuangalia hali hii kinaitwa sperm analysis.

Virutubisho
1.Zinc
Hiki ni kirutubisho muhimu sana kwa mwanaume kuweza kutungisha mimba. Kinasaidia yafatayo
1.Kuongeza kiwango cha hormone ya testosterone
2.Kuongeza idadi ya mbegu za kiume
3.Inahusika sana kutengeneza ganda au layer inayozunguka mbegu za kiume na mkia wake
4.Inahusika kuongeza uwezo wa mbegu za kiume kutembea

2.vitamin c
Hizi zinasaidia yafatayo
1.Kuzuia mbegu kushikana au kugandamana hivyo kuweza kutembea vzr
2.Kuongezea uwezo wa mbegu kukua na kukomaa vzr
3.Kuziongezea kasi mbegu
4.Upungufu wa vitamin C mwilini hupelekea mbegu kuwa na umbo lisilo la kawaida ( abnormal morphology)

3.Coenzyme Q10
 Kinasaidia yafatayo
1.Kuongeza kiwango cha hormone ya testosterone
2.Kuongeza idadi ya mbegu za kiume
3.Inahusika sana kutengeneza ganda au layer inayozunguka mbegu za kiume na mkia wake
4.Inahusika kuongeza uwezo wa mbegu za kiume kutembea

4.Viatamin E
Hii inasaidia kuongeza idadi ya mbegu,kukomaa, na kuongeze uwezo wa kutembea
Pia inasaidia kuiongezea mbegu uwezo wa kupenya kuingia kwenye yai.
Inasaidia kuzikinga mbegu na radikali huru ( free radicals) zisiziharibu

5. Vitamin D
Inasaidia kutengenezwa vzuri kwa nucleus ya mbegu za kiume.kama tunavojua hii ndo sehemu ya mbegu inayobeba DNA,pia inaongeza idadi ya mbegu

6. Selenium (Sodium Selenate)
Hii inasaidia mbegu kukomaa, kuingeza idadi ya mbegu na kuimarisha kuta za sehemu mbegu zinapotunzwa pindi zinapotengenezwa ( epididymis)

7. Vitamin B12 (Methylcobalamin)
Hii pia inasaidia utengenezwaji wa nucleus ya mbegu za kiume, upungufu wa kirutubisho hiki inaweza kusababisha mapungufu kwenye vinasaba

8. Folic Acid
Hii inasaidia kuongeza kiwango cha mbegu, na kuziwezesha kutembea.

9 Manganese (Sulfate)
Inaongeza idadi na uwezo wa mbegu kutembea na kupenya kwenye yai.

Vinapatikanaje Virutubisho Hivyo
1.zinc
Mbali na kuwa muhimu kwenye mbegu pia ni nzuri kuongeza au kuimarisha mbegu za kiume.
Inapatikana kwenye
Mbegu za maboga, nyama ya ng`ombe,kuku, maharage,spinach,uyoga,maziwa na korosho

Vitamin C
Hii utaikuta kwenye matunda kama machungwa,chenza,papai,embe ,cabbage,peas,nanasi,pera, na pilipili

Vitamin.E
Hii utaipata kwenye spinach,mchicha,embe,nyanya na viazi.vitamu
Na avocado

Vitamin D utaipata kwenye Maziwa,uyoga,fish oil,mayai na mwang wa jua

Selenium
Spinach, mayai, mbegu za alizeti,nyama ya maini,kuku na maharage
Coenzyme q 10 utaipata kwenye ufuta,mbegu za alizeti ,dagaa, cabbage,
Folic acid utaipata kwenye  avocado,papai,embe,chungwa,mahindi na nafaka nyingine, maharage, maziwa,maini.