Wasanii Wa Hip Hop Duniani Wanoingiza Mkwanja Mrefu 2019

Kanye West ndio msanii wa Hip Hop duniani ambaye amelipwa mkwanja mrefu zaidi kwa mwaka 2019 kwa mujibu wa Jarida la Forbes, hii ni kuanzia June 2018 hadi June 2019.

Orodha hiyo ya (Highest Paid Hip Hop Acts) kwa mwaka huu imetoka September 19 na kushuhudia Kanye West ambaye alikuwa nafasi ya 10 mwaka jana akiingiza kiasi cha ($27.5M) amemshusha Jay-Z na kuikalia namba 1 kwa mara ya kwanza katika historia kwa kuingiza kiasi cha ($150M) sawa na Bilioni 344.7 za Kitanzania kwa mwaka huu.

Pesa hizo ambazo ni kabla ya kukatwa kodi, hazijatokana na muziki bali zimetokana na faida ya mauzo ya kampuni yake ya viatu na mavazi "Yeezy" ambayo hivi karibuni ilitajwa kufikia thamani ya ($1.5B) hadi mwishoni mwa mwaka huu.

Jay-Z nafasi ya pili akiwa na ($81M) na Top 5 imekamilishwa na Diddy, Drake na Travis Scott. Pia orodha hii imewakaribisha mahasimu wawili kwenye Rap game ya wanawake, Cardi B na Nicki Minaj

Taarifa zinasema jumla ya mkwanja ulioingizwa na wasanii wote 20 kwa mwaka huu ni Trilioni 1.9 za Kitanzania ikiwa ni ongezeko la asilimia 33 toka mwaka jana. Hii ikiwa ni ongezeko kubwa zaidi kuwahi kutokea.

List Ya 20 Bora
1. Kanye West – $150 million
2. Jay-Z – $81 million
3. Drake – $75 million
4. Diddy – $70 million
5. Travis Scott – $58 million
6. Eminem – $50 million
7. DJ Khaled – $40 million
8. Kendrick Lamar – $38.5 million
9. Migos – $36 million
10. Childish Gambino – $35 million
11. J. Cole – $31 million
12. Nicki Minaj – $29 million
13. Cardi B – $28 million
14. Swizz Beatz – $23 million
15. Meek Mill – $21 million
16. Birdman – $20 million
17. Future – $19.5 million
18. Nas – $19 million
19. Wiz Khalifa – $18.5 million
20. Pitbull – $18 million


EmoticonEmoticon