Ya Kuyajua Kuhusiana Na Simu Mpya Za iPhone 11, Pro & Max (PICHA & VIDEO)


Kama utakuwa umegundua kwa sasa moja ya vita kubwa kiushindani katika simu janja ni eneo la kamera. 
Simu ya iPhone 11 inakuja na mfumo unaotumia kamera mbili zote zikiwa ni za megapixel 12 kila moja. 
Kamera hizi kwa pamoja zinahakikisha picha zinakuwa katika ubora mzuri ata kama ni picha ambazo zinahusisha sehemu pana sana (wide & ultra-wide).
Hata kamera ya selfi pia ni ya pixel 12 ila kwa mara ya kwanza kwa iPhone utaweza kurekodi video za 4K kwenye kamera ya selfi.  

Simu hii itaanza kupatikana kwa bei ya dola $699 (Takribani Tsh 1,600,000/=).

 iPhone 11 Pro na iPhone 11 Pro Max.
Simu hizi mbili ni simu ambazo wamezipa uwezo mkubwa sana wa kiutendaji kiasi ya kwamba Apple wanaamini zina nguvu/uwezo mkubwa kiutendaji kuliko ata laptop nyingi zinazopatikana sokoni kwa sasa. 
Hii ni kutokana na utumiaji wa chip/prosesa yao mpya kabisa ya A13, pia nje ya zile kamera mbili kama kwenye toleo la iPhone 11, hizi simu mbili zinakuja na kamera ya tatu inayozidi kuongeza ubora wa picha zake (telephoto lens).
Display ya simu hizi ni ya kiwango cha juu ya 4K – teknolojia na kiwango walichokipa jina la Super Retina OLED. 
iPhone 11 Pro ikiwa na display ya inchi 5.8 wakati iPhone 11 Pro Max ikiwa na display ya inchi 6.5.

Bei: iPhone 11 Pro inaanzisha dola $999 (Takribani Tsh 2,300,000/=) wakati iPhone 11 Pro Max inaanzisha dola $1099 (Tsh 2,530,000/=).
Simu za iPhone 11 mpya zitaanza kupatikana tarehe 20 mwezi huu (Septemba).
 Kuelewa Zaidi Unaweza kutazama Video 3 Hapo chini Nimekuwekea

iPhone 11 Pro

iPhone 11Video Inayojumuisha Matukio Yote Ya iPhone 11 & Pro


EmoticonEmoticon