CR7 Aweka Rekodi Mpya Juventus

Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo ameweka rekodi nyingine ya ufungaji katika Ligi ya Mabingwa baada ya kufunga dhidi ya Bayer Leverkusen usiku wa Oct 1.

Ronaldo alifunga bao dakika 88, katika ushindi wa mabao 3-0 iliyopata Juventus katika mchezo wa Kundi D uliofanyika kwenye Uwanja Allianz.

Bao hilo la Ronaldo linamfanya nyota huyo kufunga dhidi ya timu 33 katika Ligi ya Mabingwa akifikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Raul.

Ronaldo haiwezi kujisahau kwa rekodi hiyo kwa sababu mshindani wake mkubwa Lionel Messi naye amezifunga timu 32 katika mashindano hayo.
Cristiano Ronaldo
Nyota huyo wa Barcelona anaweza kuifikia rekodi ya Ronaldo hata leo iwapo atafunga wakati Barcelona ikivaa Inter – timu ambayo Messi hajawahi kuifunga.

Kwa sasa Ronaldo akili yake ni kuhakikisha anaisaidia Juventus kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo msimu wa 1995-96.

Msimu uliopita Juventus iliduwazwa kwa kutolewa na Ajax katika robo fainali, pamoja na Ronaldo kufunga katika michezo yote miwili.


EmoticonEmoticon