
Mtoto anapitia mabadiliko mbali
mbali ya kimwili,kiakili na kisaikolojia pindi anapokua anakuwa hadi kuwa mtu
mzima. leo nitakuelezea hatua za ukuaji wa mtoto kisaikolojia muhimu sana
katika malezi yake.
hatua hizo ni kama ifatavyo
hatua hizo ni kama ifatavyo
1.ORAL STAGE
Mtoto
anakua katika stage hii anapokuwa na umri wa,mwezi mmoja hadi mwaka mmoja.
Sasa
kwa kipindi hiki erogenous zone ya mtoto inakua mdomoni, raha ya mtoto inakua
kitu chochote kinachoingia mdomoni ndo maaana kipindi hiki mtoto kila kitu
anachoshika anapeleka mdomoni
Hiki
ndo kipindi cha kujenga strong bond kwa mtoto na mama pale mtoto anapokuwa
ananyonya inamjenga kumthamini mama kuliko mtu yyte
Kipindi
hiki inabidi kuwa makini na vitu kama shanga,sarafu nk ambavyo akiweka mdomoni
vinaweza kumkaba
Hapa
kama mzazi ana tabia ya kula kucha ndo kipindi mtoto nae anajifunza na kua hivyo
anapokua
2.ANAL STAGE
Stage
hii inaanza umri wa mwaka 1 hadi miaka mitatu
Hapa
mtoto raha yake ni kitu kinachotoka kupitia haja kubwa. Kipindi hiki ndo kile
mtoto anapenda penda sana kuomba poti au kukalia poti.
Kipindi
hiki ni kizur kumfundisha mtoto matumizi mazuri ya choo (toilet behavior s)
anapojisaidia ovyo unajaribu kumwelezea wapi pa kujisaidia nk.
Ni
stage pia ambayo unamfudisha mtoto asiwe na tabia ya kujinyea anapokua.
3.PHALLIC STAGE
Hapa
erogenous zone zinakua sehemu za siri.
Kipindi
hiki mtoto anaelewa tofaut ya kimaumbile ya mwanaume na mwanamke
Kipindi
hiki mtoto wa kike anamwonea wivu mama kwa nini anapendwa na baba na,wa kiume
anamwonea wivu baba.
Mtoto
anaanza kufanya vitu anavopendelea kufanya mzazi wa jinsia yake kwa kudhani kuwa
mzazi wa jinsia tofauti na yake ndo vitu hivyo vinafanya ampende. Unaweza kuta
mtoto wa kiume kama baba anapenda kusoma gazeti nae anapendelea kushika gazeti
kujaribu kusoma nk, au wa kike unakuta yuko busy anaigiza kujipodoa kama mama
yake nk.
Kipindi
hiki ni kizuri kumfundisha mtoto kazi fulani unayopenda akikua afanye
Pia
ni kipindi mtoto anasoma na zile tabia mbaya za wazazi, mfano kama baba anampiga
mama basi na mtoto wa kiume anajifunza akikua anakua anawatreat hivyo wanawake.
Ni kipindi cha kuacha au kificha tabia mbaya za wazazi
Phallic
stage inaanzia umri wa miaka mitatu hadi umri wa,kubarehe
4.Genital stage
Kuanzia
balehe hadi kufa
Hapa
sasa mtu anakua kimawazo na anaanza kuapply kwenye maisha yake vitu
alivyojifunza kwenye phallic stage
EmoticonEmoticon