Kwa Sababu Za Kiusalama Inakupasa Kuondoa Apps Hizi Kwenye Simu Yako Mapema

Watumiaji wa Android wamepewa orodha ya apps za kuziondoa kwenye simu zao kwa sababu za kiusalama wa data na kuondoa matangazo yanayotokea sehemu zisizohusika kwenye simu zao.

Ushauri huo umetolewa na watafiti kutoka ESET ambao wamegundua app 42 kwenye soko la Google Play Store ambazo zimekuwa zinakuja na mfumo wa kimatangazo usio rasmi – adware. 

Mfumo huo una sababisha betri ya simu kuisha haraka, utumiaji wa data – intaneti na ata kuchukua taarifa zako binafsi kwenye simu.

Baada ya utafiti wa ESET kuweka wazi Google waliondoa apps hizo kwenye soko lao la Apps, ila inakuhitaji wewe kuziondoa mwenyewe. 

Pia kuzifahamu ni muhimu kwa watu ambao wanatumia masoko mengine ya apps nje ya soko la Google Play Store. Apps hizo zimepakuliwa zaidi ya mara milioni 8.
Mfano wa Apps zinavyokuwa kwenye simu
Apps hizo ni: Smart Gallery, SaveInsta, Mini lite for Facebook, Free Radio FM Online, Free Video Downloader, Free social video downloader, File Downloader, Water Drink Reminder, Smart Notes for You, DU Recorder, Tank classic, Heroes Jump, Solucionario, Ringtone Maker, Video downloader, Ringtone Maker Pro, Basketball Perfect Shot, HikeTop+, MP4 video downloader, Flat Music Player, Free Top Video Downloader.

Apps hizo zinauwezo wa kuonyesha matangazo hata kama simu imefungwa (locked) kitu ambacho huwa kinapingwa na Google, kwani kufanya hivyo kuna sababisha utumiaji mkubwa wa betri na nje ya makubaliano yao na watengenezaji wa apps.

Baadhi ya apps hizo zipo pia kwenye soko la apps la iOS kwa ajili ya simu za iPhone ila inaonekana kwa iPhone bado apps hizo hazifanikiwa kuwa athari kubwa ukilinganisha na kwenye simu za Android.


EmoticonEmoticon