Mjadala Juu Ya Taarifa Mpya Ya Ulaji Wa Nyama

Nyama Choma
Utafiti wenye utata unasema kupunguza kula nyama, soseji, nyama ya kusagwa ni kupoteza wakati kwa watu wengi.
Utafiti huo ambao unatofautiana na tafiti za awali zilizofanywa na mashirika makubwa duniani- unasema kuna ushahidi mdogo kuwa ulaji nyama husababisha athari za kiafya.
Baadhi ya wataalamu wamepongeza "utafiti" huo lakini wengine wanahofia huenda "ukawaweka watu hatarini"
Nyama Sagwa & Sausage
Kula zaidi ya vipande vinne vya nyama zilizopitia viwandani zaidi ya mara nne kwa wiki ni hatari, ulibaini uchunguzi wa awali uliofanywa miongoni mwa watu 1,000 nchini Ufaransa, na kuchapishwa kwenye jarida la Thorax.
Watafiti wanaamini kuwa hueda sababu ya matatizo hayo ikawa ni matumizi ya kemikali ya nitrite inayowekwa kwenye nyama hizo kuzizuwia kuoza ambayo hutumiwa kwenye vyakula kama Soseji , na samaki (salami).
Lakini wataalam wanasema kuwa uhusiano wa hatari hizo haujaidhinishwa na uchunguzi zaidi unahitajika kufanyika kuthibitisha hilo.
Nyama Choma na Kachumbari
Ulaji nyama kupita kiasi umetajwa kuwa chanzo cha saratani ya utumbo.
Shirika la Kimataifa linalofanya utafiti wa saratani liligonga vichwa vya habari wakati iliposema kuwa nyama husababisha saratani.
Pia ilisema kuwa nyama nyekundu huenda ikasababisha magonjwa lakini hakuna ushahidi wa kutosha.


EmoticonEmoticon