R Kelly Apatwa Na Tatizo La Kiafya Akiwa Gerezani

R. Kelly na jaribio la pili la kutaka kukaa mbali na Jela, ameripotiwa kutetereka kiafya na anaiomba mahakama imuachie akapatiwe matibabu.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizodakwa na mtandao wa TMZ, wakili wake bwana Steve Greenberg amesema mteja wake (R. Kelly) mwenye umri wa miaka 52 anapitia tabu kwani Afya yake haipo sawa na anaumwa. 

Steve ameainisha kwamba Kellz anapatwa na Ganzi katika moja ya mkono wake. Lalamiko kubwa ni kutopatiwa matibabu stahiki.

Kellz yupo katika Jela ya mjini Chicago akisubiri kusikilizwa kwa mashtaka yake lukuki ya Unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wenye umri mdogo.


EmoticonEmoticon