Rio Fernando Amtaka Kane Afungashe Virago

Harry Kane
Rio Ferdinand amezidi kumsisitizia straika Harry Kane kwamba akusanye virago vyake na kuachana na Tottenham Hotspur kwa sababu inampotezea tu wakati.

Beki huyo wa zamani wa Manchester United, Rio amemtaka Kane kuachana na Spurs ili kwenda kujiunga na timu itakayompa fursa ya kubeba mataji kama yeye alipofanya hivyo alipoachana na Leeds United.

Kane hajashinda taji lolote kubwa tangu alipojiunga na Spurs ambapo msimu uliopita kikosi hicho kilichapwa kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mara ya mwisho, Spurs kubeba taji ilikuwa mwaka 2008 wakati walipowapiga Chelsea kwenye fainali ya Kombe la Ligi.

Na Ferdinand anamwambia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kuachana na Spurs kabla muda haujamtupa mkono.

Akisema kabla ya Spurs kuchapwa 7-2 na Bayern Munich kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ferdinand alisema: "Mi namtazama Harry Kane tu.
Harry Kane akiwa kwenye mazoezi
"Hivi unahitaji nini kwenye mpira? Unataka kuwa mchezaji aliyecheza timu moja au unataka kushinda mataji? Hivi hawa Spurs wanaonekana kuwa ni timu yenye uwezo wa kubeba mataji kweli? Sidhani. Ni wazuri, lakini hawana huo uwezo."

Kutokana na hilo, Ferdinand anamtaka Kane kufuata nyayo zake kama yeye alivyofanya huko nyuma, ambapo miaka yake 12 aliyokwenda kudumu kwenye kikosi cha Man United ilimfanya kubeba mataji kibao baada ya kuchukua uamuzi wa kuachana na Leeds United.

Kwenye kikosi cha Man United, Rio alicheza mechi 454, akifunga mabao manane na kushinda mataji sita ya Ligi Kuu England, mawili ya Kombe la Ligi na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya.


EmoticonEmoticon