Travis Scott, Kylie Jenner Wameachana

Travis Scott na Kylie Jenner wameachana na hii ni kwa mujubu wa ripoti toka mtandao wa TMZ.

Watu wa karibu wameueleza mtandao huo kwamba Wawili hao wamejaribu sana kuwekana sawa kwa muda zaidi ya week moja lakini imeshindikana, uamuzi uliofuata ni kuachana!

Imesemekana kuwa wawili hao hawakuwa na maelewano kwa kipindi hichi kifupi ambapo imeonyesha kwenye instagram ya Kylie Jenner aliacha kumpost Travis kwenye mtandao huo toka September 18.

Tayari wana mtoto mmoja Stormi Webster mwenye umri wa mwaka Mmoja.


EmoticonEmoticon