Utafiti Mpya Uliobainika Kwenye Supu Ya Pweza

Mchuzi wa Pweza

Pweza n na supu yake ni chakula cha kitamaduni tangu kale kinachopendwa na wakazi wa maeneo ya mwambao wa bahari ya Hindi , baadhi wakidai samaki huyo ni zaidi ya kitoweo, lakini je wataalamu wa lishe wanasemaje kuhusu kitoweo hiki?, Paula Odek alisafiri hadi visiwani Zanzibar kubaini mengi zaidi juu ya Pweza.
Katika utamaduni hasa wa wapwani supu ya samaki huyu hupendwa sana na kumekuwa na imani kuwa supu yake si supu tu ya kawaida kama ulizowahi kunywa.
Nyama Ya Pweza
Pweza ni kiumbe wa baharini kama vile samaki wengine,ngisi,taa na papa ,lakini ni kiumbe nadra sana anayependwa zaidi kama kitoweo miongoni mwa wakazi wa maeneo ya pwani ya bahari ya Hindi.
Kulingana na afisa wa masuala ya lishe katika wizara ya afya kisiwani Zanzibar Subira Ali, pweza ni muhimu kwa afya na lishe ya mwanadamu kutokana na virutubisho alivyonavyo.
''Pweza ana madini joto (Iodine) yanoyosaidia katika maswala ya uzazi kwa mwanamke na wanaume''. Aliniambia Bi Subra Ali.
Supu Ya Pweza
Pweza ana protini ambayo inasaidia kujenga mwili na kuweka kinga mwilini na kujikinga na aina mbali mbali za saratani na huongeza damu mwilini kutokana na chembechembe nyekundu za damu anayoitoa.
Hata hivyo Bi Subra Ali aliniambia kwamba vijana wengi wameipatia jina la supu ya pweza 'mkuyati' kwamba hunasaidia kuongeza nguvu za kiume lakini amesema ni kutokana na virutubisho alivyonavyo pweza huyo.
Pweza
Pweza hana madhara yoyote ya kiafya kwa mwanadamu na badalaya yake akinamama ambao hawana maziwa ya kutosha ya kuwanyonyesha watoto wanashauriwa na Bi Subra kunywa supu ya pweza ili ambayo anasema inasaidia kuzalisha maziwa ya mama kwa wingi kutokana na virutubisho vya protini, na madini ya chuma ambayo husaidia uzalishaji wa haraka wa maziwa kwa mama.


EmoticonEmoticon