Biashara Za Drake Zaanza Kufungwa. Amefilisika?

Mgahawa wa Drake uitwao Pick 6ix uliopo mitaa ya Toronto nchini kwao Canada umefungwa kutokana na mmiliki wake ambaye ni rapa huyo kushindwa kulipa Kodi.

Wahudumu waliweka 'Notice' kwenye mlango usiku wa November 18 isemayo, Mgahawa utafunga milango yake mpaka hapo mtakapo taarifiwa. 

Kisha Alhamis ya (November 21), wamiliki wa jengo hilo waliibuka na 'notice' isemayo kwamba wamefunga mgahawa huo na wamevunja mkataba wa kupangishana kutokana na kushindwa kulipa Kodi.

Andiko hilo la kuvunja mkataba unaonesha deni ambalo linadaiwa ni milioni 155 za Kitanzania. Licha ya kuwasiliana kwa muda mrefu na Chubbs ambaye ni mshirika kibiashara na Drake, mmiliki huyo amesema hakufanikiwa kupata fedha hiyo.


EmoticonEmoticon