Jose Mourinho Atoa Sababu Za Kumshukuru Dogo Muokota Mipira

Jose & Ball Boy
Jose Mourinho amemwagia sifa muokota mipira uwanjani 'ball boy' kwa kuwa sehemu ya bao muhimu lililofungwa na Harry Kane katika mchezo wa jana Jumanne usiku  dhidi ya Olympiacos.

Wakati ambao Tottenham  walikuwa nyuma mabao 2-1, kijana muokota mipira, alifanya kwa haraka kumpa mpira uliokuwa umetoka, Serge Aurier.
Jose Mourinho
Aurier naye alimrushia Lucas Moura wakati huo mabeki wakiwa wamezubaa, walistuka akiwa anapiga krosi iliyomaliziwa na Kane ambaye aliifungia Tottenham waliokuwa nyumbani bao la kusawazisha.

Baada ya kumalizika mchezo huo ambao Tottenham  waliibuka na ushindi wa mabao 4-2, Mourinho alisema, "Nimependa alichofanya yule kijana. Aliuelewa mchezo na kutoa msaada,".
Harry Kane
Olympiacos walianza kuitangulia Tottenham  mabao mawili ya haraka yaliyofungwa na  Youssef El-Arabi na  Ruben Semedo kabla ya kujisawazishia katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kupitia Dele Alli na  Kane.


EmoticonEmoticon