Justin Biber Ampa Mke Wake Zawadi Ya Milion 150 Kwaajili Birthday

Justin Na Hailey
Miaka 23 ya mrembo Hailey Baldwin imekuwa na baraka tele kwani amefanikiwa kufunga ndoa na Justin Bieber mwezi September, JB amemshangaza mke wake huyo kwa zawadi nzuri na ya gharama Kubwa.

Bieber alianza kwa kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa mke wake kwa kumuandikia ujumbe ambao aliumaliza kwa kusema 'Next Season BABIES' ikitafsiriwa kuwa wawili hao wapo tayari kutuletea watoto duniani kuanzia sasa.

"Happy birthday babes! You make me want to be better everyday! The way you live you life is so attractive.. ps you turn me on in every way 😍😍😍😍 next season BABIES."

Kisha akamaliza post ya pili na video ambayo inaonesha zawadi ya saa aina ya Audemars Piguet White Gold Diamond ambapo bei yake inatajwa kuwa (USD 65K) sawa na milioni 150 za Kitanzania.

Audemars Piguet ni miongoni mwa saa zenye gharama zaidi duniani kwani bei zake hufikia hadi (USD 900K) sawa na Bilioni 2 za Kitanzania kwa saa aina ya Audemars Piguet Royal Oak Grande Complication


EmoticonEmoticon