Kuna Ukweli Nanasi Linaweza Kutoa Mimba/ Madhara Kwa Mjamzito?

Kuna uvumi kwamba unapokula nanasi au juice yake inasababisha mimba kutoka au kujifungua kabla ya muda wa kujifungua kufika.
 

Sio kweli ni uvumi tu. Ndani ya nanasi kuna Bromelain. Na vidonge vya bromelain sio salama kutumika wakati wa ujauzito kwani vinapelekea mimba kuharibika. 
Ila kiwango kilochomo kwenye nanasi ni kidogo sana. Ili ufikie kiwango cha kidonge kimoja cha bromelain unahitaji kula nanasi 10 kwa wakati mmoja,unaweza ona ni kiasi kidogo cha bromelain kilichopo kwenye nanasi. 

Hivyo kula nanasi haina tatizo kwa mjamzito ila ina faida kwani ina kiwango kikubwa cha Iron na folate ambayo ni muhimu kuongeza damu. Pia ina vitamin C, Manganesse, na vitamin B6 ambavyo.ni muhimu kwa mama mjamzito


EmoticonEmoticon