Rekodi Ya Kuandikwa Kwenye Kitabu Cha Dunia Yamfikia Mariah Carey

Mwimbaji Mariah Carey ameingia kwenye rekodi ndani ya Kitabu cha Guinness World Records kupitia wimbo wake "All I Want For Christmas Is You" wa mwaka 1994 toka kwenye album yake, Merry Christmas.


Wimbo huo umeweka rekodi 3 kubwa na kumfanya Carey kukabidhiwa cheti hicho toleo la mwaka 2020.

Guinness wamesema rekodi hizo ni pamoja na; Kuvunja rekodi kwa kuwa wimbo wa Sikukuu uliokaa kwa muda mrefu zaidi kwenye Chart za Billboard Hot 100 kwa msanii mmoja yaani Solo Artist, Pia umeweka rekodi ya kuwa wimbo uliosikilizwa zaidi kwenye Spotify kwa masaa 24 kwa msanii wa Kike, ukisilizwa mara milioni 10.8 mwezi Disemba mwaka jana.

Rekodi ya mwisho ni kukaa kwa wiki nyingi zaidi kwenye Top 10 Chart za UK kwa wimbo wa Christmas, wiki 20. Mariah Carey amekabidhiwa cheti hicho kwenye show yake mjini Las Vegas.


EmoticonEmoticon