T.I Atolea Ufafanuzi Suala La Kumwangalia Mwanaye Bikra

T.I
Rapper Clifford Harris Jr.,alimaarufu T.I na mkewe, Tameka “Tiny” Harris, wamekaa na mkewe Tiny Harris pamoja na Jada Pinkett Smith kwenye kipindi cha “Red Table Talk” na kulitolea ufafanuzi suala lake lililolaaniwa dunia kote  kwamba huwa anatabia ya kumpeleka binti yake Deyjah Harris kwa daktari wa wanawake kumuangalia kama bado ana usichana wake.

T.I alisema “Maana yangu ilitafsiriwa tofauti, acha niweke mambo sawa. Sikusema kwamba nilikuwa naingia naye kwenye chumba cha daktari. 
Hiyo ni kunitafsiri vibaya. Huo ni Uongo. Na pia sikusema ķwamba huwa ninafanya hilo kwa siku hizi, kwa sababu tayari ana umri wa miaka 18. 
Na sikusema ķwamba mama yake anakuwa hayupo, mama yake huwa anakuwepo na kila kitu.” Ameeleza T.I.
Licha ya yote, alimuomba radhi binti yake Deyjah na pia aliweka wazi kuwa alikuwa anafanya vile wakati binti yake huyo akiwa na umri wa miaka 15 na 16 lakini kwa sasa haipo tena hivyo.
Kama utakumbuka mahojiano yale ya T.I. na Podcast ya “Ladies Like Us” ya Nazanin Mandi na Nadia Mohan yaliyoibua sakata hili yalifutwa mtandaoni lakini athari ilikuwa kubwa hadi kupelekea Deyjah kum-unfollow baba yake mzazi na hata pia baadaye kuzifuta akaunti zake za mitandao ya kijamii.


EmoticonEmoticon