Unai Emery Abebeshwa Virago Na Arsenal, Kikosi Cha Arsenal Kipo Chini Ya Huyu...

Unai Emery
Unai Emery amefutwa kazi na Arsenal baada ya kuinoa timu hiyo kwenye miezi 18 tu.

Mhispaniola huyo,ambaye aliongoza Paris Saint-Germain kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ufaransa na kushinda mataji matatu ya Europa Leagues akiwa na Sevilla, aliteuliwa kuwa kocha wa Arsenal Mei 2018, alipotua Emirates kurithi mikoba ya Arsene Wenger.

Na sasa kikosi hicho cha Emirates kitakuwa chini ya Freddie Ljungberg kwa kipindi cha mpito. 
Freddie Ljungberg
Arsenal wamesema kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kutofurahishwa na matokeo ya uwanjanni na kiwango cha timu kwamba haichezi kwenye ubora unaotakiwa.

Arsenal imeshindwa kupata ushindi kwenye mechi saba mfululizo na kipigo cha mabao 2-1 nyumbani uwanjani Emirates kutoka kwa Eintracht Frankfurt kwenye Europa League Alhamisi ndicho kilichofikisha mwisho ajira ya Mhispaniola huyo.

Arsenal haijashinda kwenye Ligi Kuu England tangu Oktoba 6 na sasa wapo nyuma kwa pointi nane kuifikia Top Four, ambayo ndio msingi mkuu wa timu hiyo kwa msimu huu katika kuifukuzia nafasi ya kurudi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kukosa kwa misimu kadhaa.


EmoticonEmoticon