Wataalamu Wasema Kiwango Cha Nyuzi Joto Kuongezeka Kwa Kasi

Wataalamu wa mazingira wa kimataifa wameonya kuwa nyuzi joto duniani zinaweza kupanda kwa kiwango cha juu katika karne hii na kusababisha madhara mbali mbali na uharibifu baada ya gesi zinazoharibu mazingira kufikia viwango vya juu kabisa mwaka jana.

Mkuu wa shirika la dunia la utabiri wa hali ya hewa amesema nyuzi joto duniani zinaweza kupanda kwa nyuzi joto 3 hadi 5 Celsius juu ya kiwango kilichokuwapo kabla ya enzi ya viwanda karne hii, zaidi ya mara tatu katika kiwango kilichokubalika, iwapo hakuna kitu kitakachofanywa kuzuwia kupanda huko.

Utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira umeongezeka kwa kiwango cha juu kabisa mwaka jana, Umoja wa Mataifa umesema katika ripoti yake ya pengo la utoaji gesi hizo, iliyotolewa kabla ya mkutano wa mazingira wa Umoja wa mataifa mjini Madrid wiki ijayo kuzuwia ongezeko la utoaji wa gesi hizo.


EmoticonEmoticon