Zijue Athari Za Sumu Kuvu Kwa Binaadamu

Serikali za Kenya,Uganda na Rwanda zimepiga marufuku bidhaa kadhaa kama vile baadhi ya unga wa mahindi na siagi ya karanga baada ya vipimo kuonyesha kuwa zina viwango vya juu sana vya sumu kuvu ama aflatoxin
Hatua hii imeashtua wengi haswa watumiaji wa unga wa mahindi unaotumika kupiga Ugali ama sima. Ugali ni chakula kinachopendwa sana na watu wengi haswa Afrika Mashariki.
Kulingana na shirika la Afya Duniani(WHO), sumu kuvu huharibu karibu asilimia 25 au zaidi ya chakula kinachozalishwa duniani kila mwaka.
Je sumukuvu ni nini?
Sumu kuvu ni familia ya sumu zinazozalishwa na kuvu zinazopatikana kwa mimea inayopandwa kama vile mahindi,karanga,pamba na kadhalika.Kuvu mbili zinazochangia kuzalisha sumukuvu hufanya vizuri sehemu zilizo na joto na unyevu.
Sumu kuvu huathiri mimea iliyoko kwenye shamba,wakati wa kuvuna na hata wakati wa kuhifadhi mazao ya mimea baada ya kuvuna.
Sumu kuvu huweza kukaa kwenye mchanga na hivyo kuvutwa sawia na rutuba wakati mimea mingine inapopandwa na kuanza kukua.
Watu wanaweza kupata sumu kuvu wanapokula mimea iliyoathirika na sumu hii au hata nyama ama bidhaa za maziwa kutoka kwa wanyama waliokula mimea yenye sumu hiyo.
Wakulima pamoja na wafanyikazi wa shambani wanaweza kuathiriwa pia na sumu kuvu kwa kunusa vumbi inayotokana na mazao yalioathiriwa na sumu kuvu wakati wanaposhughulikia mazao.
Athari za sumukuvu
Kula chakula kilicho na zaidi ya Miligramu 1 kwa kila kilo moja kunaweza kusababisha ugonjwa wa 'aflatoxicos'
Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kutapika,kuumwa na tumbo,kuwa na maji kwenye mapafu na kuharibikwa kwa maini.
Kulingana na David Osogo,mtafiti wa lishe na afya katika Shirika la Africa Population Health Research Center jijini Nairobi,si dhana, ni jambo linalofahamika kuwa sumu kuvu huzalisha kemikali mwilini ambazo husababisha saratasi ya ini.

SOURCE:BBC SWAHILI


EmoticonEmoticon