Zuia Mtu Yeyote Kukuweka Kwenye Whatsapp Group Bila Ruhusa Yako

Ingia kwenye programu yako ya WhatsApp kisha bofya sehemu ya Settings > Account > Privacy > kisha chagua menu mpya iliyoandikwa Groups

Hapo utaweza kuona Menu mpya yenye Maelezo yenye kutaka uchague ni nani atakaye weza kukualika kwenye magroup ya WhatsApp.

Kila sehemu inayo maana yeka na ni muhimu kuzingatia ni menu unayochangua ili kuweza kuzuia watu sahihi kukualika kwenye magroup.

Everyone – Pale utakapo changua sehemu hii utaweza kuruhusu watu wote kukualika kwenye magroup ya WhatsApp na hii ndio Menu inayokuwepo mara unapo ingia kwenye ukurasa huu.

My Contacts -Pale utakapo chagua menu hii utaweza kuruhusu watu wote ulio save namba zao kwenye simu yako kuweza kukualika kwenye magroup ya WhatsApp.

My Contacts Except -Hapa utaweza kuchagua ni watu gani au mtu gani mmoja au zaidi wataweza kukualika kwenye magroup ya WhatsApp, hapa unaweza kuzuia watu wote kwa kuchagua alama ya tiki iliyopo juu upande wa kulia ndani ya majina yatakayo funguka baada ya kuchagua sehemu hiyo.
Hata hivyo watu wote ambao watakua hawana uwezo wa kukualika kwenye magroup wataruhusiwa kukutumia meseji binafsi, meseji ambayo itakuwa na uwezo wa kudumu hadi siku tatu na baadae kuacha kufanya kazi.

Kwa sasa tayari sehemu hii inapatikana kwa watumiaji wa programu ya WhatsApp ya Android na iOS na unaweza kupata sehemu hii kama unatumia toleo jipya la programu ya WhatsApp.


EmoticonEmoticon