Alilolifanya Jay-Z Kwenye Birthday Ya Kufikisha Umri Wa Miaka 50

December 4 Rapa Jay-Z ametimiza umri wa miaka 50, ana rekodi ya kushinda Tuzo 22 za GRAMMY, yupo kwenye 100 bora ya Wasanii bora wa dunia kwa mujibu wa billboard, pia ni Bilionea Mwana-Hiphop wa kwanza.

Kuadhimisha siku hiyo, Jay-Z amerudisha album zake zote kwenye mtandao hasimu wa Spotify. Kumbuka Jigga ni mmiliki wa mtandao wa TIDAL ambao pia unafanya vizuri kwenye kusikiliza na kupakua muziki wa wasanii mtandaoni.
Jay-Z aliziondoa album hizo 9 kati ya 12 mwezi April mwaka 2017 na kufanya zipatikane Exclusively kwenye TIDAL.

Anashikilia pia rekodi ya kuwa Muamerika mweusi namba tatu kwa utajiri, Yeye na Ndugu zake Watatu walilelewa na Mama yao baada ya Baba kuitelekeza familia.

Jigga ambae aliwahi kuja Tanzania mwaka 2006, tukio la ajabu alilowahi kulifanya ni kumpiga risasi ya bega Kaka yake kutokana na kumuibia vito vya thamani. 


EmoticonEmoticon