Cardi B Amtetea Offset Baada Ya Ushahidi Wa Kumtongoza Mwanamke Mwingine Kuthibitika

Offset amerudi kwenye kashfa ya kumsaliti mkewe Cardi B. Leo limeibuka jipya tena na mpenzi wa Tekashi 69, aitwaye Jade.

Unakumbuka Cardi B anashtaka la kuwashambulia wanawake wawili, Baddie G na Jade kwa kuhisi wanatoka na mumewe? Kabla halijapoa hilo, Offset amemcheki Jade tena DM na kumwambia amem-miss (Miss U fr)

Jade ndiye amemwaga mchele huo hadharani na kuandika kwamba "Mkeo Cardi ana shtaka la uhalifu. Kwanini unanitumia ujumbe mimi, hauna heshima kwake? Kuna vitu vingi ambavyo sijaviweka wazi bado, lakini kuna muda wake tu." Aliandika mpenzi huyo wa rapper Tekashi 69 


Sasa ni Cardi B ambaye amekuwa wa kwanza kuibuka na kumtetea mumewe, amedai kuwa Akaunti ya instagram ya Offset imedukuliwa, na mumewe hawezi kufanya ujinga huo.

Status Za Mke Wa Takesh 69
Watu wote wanajua aliwahi kufanya upuuzi kipindi cha nyuma lakini kwa sasa, sio mjinga kiasi hicho tena. Wapo vizuri na wanafuraha.

Cardi B ameeleza hayo kwenye video kadhaa ambazo aliziweka kwenye instagram akaunti yake asubuhi ya leo na tayari ameziondoa.


EmoticonEmoticon