Cristiano Ronaldo Akataa Unahodha Juventus

Mshambuliaji wa Juventus ya Italia Cristiano Ronaldo amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii kufuatia uamuzi wake wa kukataa kuvaa kitambaa cha unaodha katika mchezo wa Juventus dhidi ya Udenise wa Ligi Kuu ya nchini Italia (Serie A), waliopata ushindi wa 3-1 na kuifikia Inter Milan kwa kuwa nao sawa kwa point 39 ila Inter akiongoza kwa tofauti ya magoli.
Kitambaa cha unahodha katika mchezo huo kilivaliwa na Leonardo Bonucci  lakini baada ya kufanyiwa mabadiliko akampa kitambaa hicho Gonzalo Higuan ambaye nae dakika 5 baadae akatolewa ndipo akaenda kumpatia kitambaa cha unahodha Cristiano Ronaldo na kukikataa.
Ronaldo alikichukua kitambaa hicho na kwenda kumvalisha mchezaji mwenzake Blaise Matuidi  kama heshima kutokana na mchezaji huyo kucheza Juventus kwa muda mrefu, hivyo inadaiwa Ronaldo hakuona kama anastahili kuvaa kitambaa mbele ya Blaise Matuidi aliyemkuta katika club hiyo wakipishana mwaka mmoja (Ronaldo 2018, Matuidi 2017 akitokea PSG)


EmoticonEmoticon