Cristiano Ronaldo Atia Neno Endapo Wakikutana Uwanjani Na Real Madrid, kiwango Kimeshuka

Mshambuliaji wa timu ya Juventus, Cristiano Ronaldo, ameweka wazi kuwa hataki kukutana na timu yake ya zamani Real Madrid kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora.

Juventus wamemaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi la A, huku Real Madrid wao wakimaliza nafasi ya pili kwenye kundi A, hivyo dro ya hatua ya 16 bora inatarajiwa kupangwa Jumatatu wiki ijayo.

Amedai hatokuwa na furaha endapo atakutana na timu hiyo, lakini atafurahi kama atakuja kukutana kwenye mchezo wa fainali huko Uturuki, Mei mwakani.
“Real Madrid ni timu bora duniani, lakini kwa sasa sipendi kukutana nao kwa kuwa itakuwa mapema sana, nimeondoka hapo hivi karibuni, hivyo kukutana nao tena siku za hivi karibuni itakuwa ngumu kwangu, Bado ninawakumbuka wachezaji ambao nimekuwa nao kwa kipindi kirefu ndani ya kikosi hicho, hivyo ni vizuri nikaja kukutana nao kwenye mchezo wa fainali kwa kuwa itakuwa haina nanma, ila kwa sasa itaniumiza sana,” alisema Ronaldo.
Hata hivyo Ronaldo msimu huu bado hajaonekana kuwa kwenye kiwango kizuri kama wakati anakipiga ndani ya klabu ya Real Madrid.
Katika michezo kadhaa iliopita mchezaji huyo amekuwa akitolewa kabla ya mchezo kumalizika jambo ambalo lilikuwa limeacha maswali mengi kwa mashabiki. 

Kocha wa timu hiyo Maurizio Sarri, aliwahi kuweka wazi kuwa amekuwa akimtoa mchezaji huyo kwenye baadhi ya michezo kutokana na kutokuwa fiti pamoja na kuwa majeruhi.


EmoticonEmoticon