Darassa Atoa Sababu Za Kufanya Wimbo Na Harmonize, Hakutegemea

Msanii wa kizazi kipya Darassa amefunguka kuhusiana na wimbo wake mpya wa Yumba kwanini ameamua kumshirikisha Harmonize na sio msanii mwingine.

Akipiga story kupitia kituo cha redio cha Clouds Fm Darassa amesema kuwa, "Jamaa ana iyo vibe, kwasababu hamna kitu napendaga kama kufanya nyimbo mnajisikia, mimi na Harmonize tulikuwa hatujapanga lini au tarehe ngapi tufanye wimbo, tulikutana studio na tukaamua tufanye wimbo.

Pia Darassa alisema kwamba kufanya kazi na Harmonize kumechangiwa na producer wake ambaye ni Abbah aliyekuwa akitamani wafanye kazi pamoja, "Unajua Harmonize ni mtu ambaye anafanya kazi zake safi na ana nguvu kwenye sanaa yake so mi niliweka uaminifu kwasababu nlisikia kitu ambacho anakifanya halafu kinahitajika kuwa kwenye wimbo wangu. na kati ya wasanii nliofanya nao kolabo na wakafanya pati zao wenyewe Harmonize ni mmoja wao na alichokuwa anakifanya niliona kweli hapa pana Art".Alimaliza Darassa

SIKILIZA YUMBA HAPA KAMA ILIKUPITA


DOWNLOAD


EmoticonEmoticon