Everton Yatia Neno Kuhusiana Na Zlatan Ibrahimovic

Everton imezungumza na ajenti Mino Raiola kumuachilia mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, ikiwa yuko tayari kuhamia Goodison Park, japo AC Milan inapigiwa upatu kumsani mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United.

Kwingineko, Manchester United imeonesha nia ya kutaka kumnunua mchezaji wa Bayer Leverkusen Mjerumani Kai Havertz, 20. Hatahivyo inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Barcelona, Liverpool, Real Madrid na Bayern Munich.


EmoticonEmoticon