Fahamu Mji Ambao Krismasi Ipo Mwaka Mzima

Mapambo ya siku kuu ya Noeli yapo kila siku katika mwaka
Katika mji wa Alaska Krismasi ipo mwaka mzima.
Binti mmoja mwenye umri wa miaka 21 anasimulia maisha ya eneo alilokulia.
Alikulia katika ncha ya kaskazini ana sasa anafanya kazi katika nyumba ya mapambo ya Krismasi.
Anasema kuwa huwa anapata tabu sana kuwaelezea marafiki zake wapya mtandaoni kuhusu mji anaoishi.
Wengi huwa wanadhani kuwa anatania na kutomwamini kwa kile anachokisema.
"Watu huwa wanahoji , kweli huo mji upo kweli? Hivyo inanibidi awaonyeshe kwenye Google kuwa ni mji wa kweli"
Kaskazini mwa Pole ndio kuna sanamu kubwa zaidi duniani ya 'Father Christmas'
Katika mji mdogo wa Kaskazini mwa Pole, eneo ambalo lina idadi ya watu 2,117 ni umbali wa kilomita 2,700 kutoka ncha ya kaskazini.
Mji huo umekuwa unavutia idadi kubwa ya watalii.
Barua nyingi huwa zinaandikwa na kupokelewa na kikundi cha vijana wanaojitolea.
Anasema kuwa ni maisha mazuri huko na ya kipekee. Baba Krismasi huwa ana kazi nyingi na huwa anapaswa kuandika barua kwa watoto duniani kote.
Na huwa anafurahia kuwajibu watoto wote wanaomwandikia barua.
Mitzi anasema kuwa anasema kuwa huwa anajibu barua zilizoandikwa na Santa kutoka duniani kote
Wakati kama huu wa mwaka, huwa kuna mwanga kila kona.
"Kwa kawaida Jua huwa linachomoza majira ya saa tano asubuhi au saa sita mchana wakati wa msimu wa baridi,"alieleza Cody. "Na jua huwa linazama majira ya saa tisa mchana, hivyo huwa tunapata saa nne kwa siku."
"Taa za krismasi au za kuonyesha shangwe huwa zinawashwa na kutumika kama mbadala wa jua," alieleza Mitzi.
Vipi kuhusu baridi? Baridi huwa linafika nyuzi joto -25° mwezi Desemba.
Je, usiku huwa unafananaje kaskazini mwa Pole? Kwa mujibu wa Cody, huwa ni burudani sana kwa watu kuangalia kile kinachoonekana nje.
"Michezo ya kuchezea barafu na kuvua samaki katika barafu hayo ndio mambo ambayo huwa yanafanyika."
Mitzi anasema kuwa Krismasi ni kipindi cha mwaka ambacho huwa anakipenda katika mwaka.
Krismasi inaweza kukaa katika mji huo hata kwa miaka miwili mfululizo.
"Mimi ninapenda Krismasi," aliongeza "Ninaweza kukaa hapa kwa muda mrefu zaidi kama sio maisha yangu yote."

By BBC


EmoticonEmoticon