Familia Ya Kanumba Yakumbwa Na Msiba Mwingine, Mama Afunguka

SETH BOSCO, mdogo wa aliyekuwa staa wa Bongo Movie, marehemu Steven Kanumba, aliyefariki usiku wa kuamkia leo, Desemba 7, 2019, baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani kwao Kimara-Temboni, jijini Dar es Salaam alipokuwa akiuguzwa kwa muda  mrefu baada ya kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo, atazikwa jijini Dar es Salaam Jumatatu wiki ijayo mahali ambapo patatangazwa baadaye.

Habari hiyo imetolewa na mama wa marehemu, Bi Flora Mtegoa, alipokutana na waandishi wa habari ambapo ameongeza kwamba Seth alifariki muda mfupi nyumbani baada ya kuongea na mama yake na watu wengine nyumbani.
“Tuliporudi nyumbani kutokea Muhimbili alikuwa yuko vizuri tu, akaomba alale kidogo kisha tumuamshe aangalie TV kwani kuna kipindi anakipenda alitaka kukiona, lakini alifariki akingali kitandani ambapo daktari tuliyekuwa naye alisema marehemu alipata shida ya kupumua,” alisema Bi Mtegoa.

Credit:Globalpublishers


EmoticonEmoticon