Fat Joe Atangaza Kustaafu Muziki (VIDEO)

Dre & Fat Joe
Rapper Fat Joe ametangaza kustaafu muziki baada ya kuhudumu kwa takribani miaka 27. Fat Joe amezungumza hayo asubuhi hii kwenye mahojiano na CBS This Morning.

Amesema album yake ijayo 'Family Ties' ambayo itatoka Disemba 6 mwaka huu ndio itakuwa ya mwisho na hatanii kama ambavyo wasanii wengine wamekuwa wakifanya na baadaye kurejea tena.

"Ni kama sipo tena kwenye hii game, Nafikiri ninastaafu. Ni muda wa kuacha sasa. Huwa ninakasirishwa na rappers ambao huwa wanasema wanastaafu halafu wanarudi tena. 

Ninalipinga hilo kwa nguvu, mimi kwa asilimia 85 tayari." Amesema Fat Joe mwenye umri wa miaka 49.

Mpaka sasa tayari ameachia jumla ya albums 10, nyimbo 22 na mixtapes 3.


EmoticonEmoticon