Forbes Watoa Top 10 Wanamichezo Waliongiza Mkwanja Mrefu 2019. Mayweather Atoa Neno

Floyd Mayweather

Mbabe wa ndondi duniani kwenye uzito wa kati kutoka nchini Marekani  Floyd Mayweather ambaye alistaafu lakini ametangaza kurejea kwenye ndondi tena ameamua kupost orodha ya wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani na yeye akiwa nambari moja akiwa ndio mwanamichezo anayelipwa pesa nyingi zaidi.Forbes ListKupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii Mayweather amepost huku akishukuru kwa kuwa mwamamichezo anayelipwa pesa nyingi kwa msimu wa tano mfululizo.Mayweather Instagram Caption
Aliandika amneno haya:- "Imethibitishwa hiyo, Kwanza nianze kwa kutoa pongezi zangu kwa kila mwanamichezo aliyopo kwenye orodha hii na pili nimeheshimu kwa kuendelea kuweka rekodi. Sio kwamba namdharau mtu yeyote lakini nimekuwa nambari moja kwa kweli katika miaka 5 mfululizo bila matangazo yeyote. Sikutaka kuwa na mpango wa kuwa na matangazo au uwekezaji wowote kutoka kwa mtu yeyote kwa sababu maono yangu yalikuwa daima kuwa bosi mimi mwenyewe na sikutaka kumuachia mtu yeyote. Kwa hivyo nilianzisha kampuni yangu mwenyewe na kukuza na chapa (Brand ) yangu mwenyewe (TMT) ambayo tunaendelea kukua na hivi karibuni watakuwa wadhamini wangu wakubwa. Unaweza kusema unataka nini juu ya Floyd Mayweather lakini nambari na matamko huchanganyika hayadanganyi. Hii kwakweli naweza kusema iko juu ya bidii na kujitolea na kujua dhamana yako mwenyewe".


EmoticonEmoticon