Frank Lampard Afunguka Majina Ya Anayotarajia Kuwasajili January

Frank Lampard
Lampard tayari ana majina yake kichwani ya wachezaji anaotaka kuwasajili kwenye dirisha la Januari baada ya kukabishiwa mkwanja wa Pauni 150 milioni kufanya vurugu sokoni.

Chelsea wameshinda rufaa yao na kuondoka kwenye kifungo cha kuzuiwa kusajili na sasa watakuwa bize kuleta sura mpya kwenye kikosi hicho cha Stamford Bridge kwenye dirisha la Januari.
Kocha Lampard atakuwa bize kufanyakazi na mkurugenzi Marina Granovskaia na mmiliki Roman Abramovich juu ya wakali wapya anaotaka watue kwenye kikosi chake, huku beki wa kushoto wa Leicester City, Ben Chilwell akidaiwa kuwa chaguo la kwanza la kocha huyo akitaka atue huko Stamford Bridge.

Lampard alisema: “Nina wachezaji wangu kichwani tayari. Lakini, wakati huo huo nakuwa na mawazo ya wachezaji waliopo kwenye timu na namna wanavyojitolea mazoezini na wanavyofanya vyema kwenye mechi.
“Haina kificho kila kocha kwenye Ligi Kuu England atakuwa muongo kama atasema hafikirii wachezaji wengi. Tunao skauti wetu, watu wetu ambao tumekuwa tukifanya nazo kabisa miaka yote. 

Mimi siendi kila sehemu au siwezi kutumia google kutafuta wachezaji wazuri wa kuwanunua."


EmoticonEmoticon