Jose Mourinho Ajitetea Baada Ya Kugundulika Amejifunza Kijerumani, Kuhamia Bayern

Jose Mourinho
Jose Mourinho anasisitiza kuwa  kujifunza kwake Kijerumani hakuna uhusiano wowote na kazi huku akiongeza kuwa hana mipango yoyote ya kuiacha Tottenham na kuhamia Bayern Munich.
Hapo awali inadaiwa kuwa Bayern walitaka kumwajiri Mourinho baada ya kumpiga kalamu Niko Kovac mwanzo wa mwezi Novemba.
Hata hiyo Mourinho baada ya wiki mbili alipata kazi yake mpya na kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino katika klabu ya Tottenham na kuiacha Bayern ikimtafuta kocha atakayechukua nafasi ya Kovac.


EmoticonEmoticon