Kauli ya Mesut Ozil Ilivypolekea Mechi Ya Arsenal Dhidi Ya Manchester City Kufutiliwa Mbali

Shirika la habari nchini China CCTV,  lilifutilia mbali kuonyesha mechi ya Arsenal dhidi ya Manchester City iliyotarajiwa kupigwa Leo disemba 15 Jumapili saa 1:30 usiku kwa muda wa Afrika Mashariki kufuatia ujumbe uliandikwa na mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil kupitia mitandao yake ya kijamii.

Ozil alichapisha aliposti ujumbe kwenye akaunti zake za kijamii ambao unakosoa namna Waislamu wa Uighurs wanavyoteswa nchini China.
Kupitia ujumbe huo, Mesut Ozil aliwaita Waislamu hao wa Uighurs kama mashujaa ambao wanapinga unyanyasaji na mateso na kuikosoa China pamoja na idadi kubwa ya Waislamu waliolifumbia macho jambo hilo.
”(Ndani ya China) Qurans zilichomwa, Miskiti ilifungwa, Shule za Kiislamu, Madrasa zilizuiliwa, Wasomi wa dini wamekuwa wakiuawa mmoja kwa mmoja. Pamoja na hayo yote Waislamu wamekaa kimya,” Ameandika Ozil ambaye ni Muislamu kupitia Twitter.

Chama cha soka nchini China kimeiyambia chombo cha habari cha Serikali kuwa kimesikitishwa na sana na matamshi yaliyotolewa na Ozil hawaungi mkono.
”Kauli ya Ozil, imewaumiza sana mashabiki wa China wanaomfuatilia, lakini wakati huo huo ujumbe wake umeumiza hisia za watu wa China. Hiki kitu hatuwezi kukikubali.” Ujumbe kutoka katika chama hicho cha soka.
Gazeti la Global Times limesema kuwa sasa CCTV-5 imeufutilia mbali kurusha matangazo ya mechi hiyo na badala yake itaonyesha mchezo wa Tottenham dhidi ya Wolves.
Hata hivyo Arsenal imesema kuwa ayihusiki na matamshi ya Kiungo huyo raia wa raia Ujerumani ikidai kuwa huwa haijihusishi na mwaswala ya kisiasa na kuongeza kuwa hayo yalikuwa maoni binafsi ya Mesut Ozil.


EmoticonEmoticon