Kauli Ya Mourinho Kuhusu Manchester United Yazua Mjadala

Jose Mourinho
Anaporejea leo Old Trafford kama mkufunzi wa Tottenham, Jose Mourinho amesisitiza kuwa yeye si hasidi wa Manchester United. 
Itakuwa ni vuta nikuvute leo ikiwa ndio mara ya kwanza Mreno huyo  kucheza dhidi ya United tangu klabu hiyo imtimue mwezi Disemba mwaka jana.
Mourinho aliiacha United ikiwa nambari 6 kwenye jedwali na furaha yake ni kwamba tangu atie guu katika kasri hiyo mpya, Tottenham imejizolea ushindi mara tatu.
Swali ni je, ni upi mustakabali wa wachezaji wa kutegemewa Tottenham?


EmoticonEmoticon