Kodi Ya Harusi Yafutwa Rasmi Baada Ya Wananchi Kususia Ndoa

Mamlaka Kaskazini mwa Nigeria zimesitisha agizo lake la kuwakata watu kodi wanapooa baada ya wananchi wa eneo hilo kupigia kelele uamuzi huo. 

Uamuzi huo ulianza baada ya bwana Ado Sa’id, ambaye ni chifu wa kijiji cha Kera kaskazini magharibi mwa Nigeria, kutangaza kuwa kila mwanaume atakayetaka kuoa atapaswa kulipa kodi ya kiasi cha dola 375 za Kimarekani(Tsh.Laki Nane, Sitini Na Moja Elfu) .

Hii ikiwa ni mbadala wa utamaduni ambao uliopo wa kulipa samani, vyombo vya jikoni na vitu vingine vya thamani kwa ajili ya kutoa kwa familia ya bibi harusi watakapofunga ndoa.
Kiongozi huyu amesema kuwa kulipa kodi ni rahisi zaidi kuliko kulipa mahari na itawafanya watu wengi kufunga ndoa kirahisi. Amri hiyo iliwafanya wakazi wa eneo hilo kushindwa kufunga ndoa


EmoticonEmoticon